Mwalimu wa shule ya Msingi Bukumbi Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Claud Makalanga (23) amehukumiwa miaka 30 jela kwa kumlawiti kwa nyakati tofauti mwanafunzi wa kiume (10) tangu mwaka 2020.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa wilaya hiyo, Amani Shao alitoa hukumu hiyo Machi 23, 2023 baada ya kusikiliza shauri la makosa ya jinai namba 103 ya mwaka 2022 Kwa pande zote.
Shahidi wa kwanza ambaye ni muathirika jina linahifadhiwa aliileza Mahakama kuwa mwaka 2020 akiwa darasani mwalimu Makalanga alimwita kwenye ofisi ya taaluma na kumlawiti huku akimuonya kutomwambie mtu na kuendelea kumfanyia kitendo hicho ambapo kila alipomaliza kumlawiti alimpa kati ya Sh5,000 hadi Sh10,000 hadi alipokmatwa mwaka 2022.
“Aliniita ofisini na kunivua kaptula na kunilawiti akanipa Sh5,000 akaniambia nisisema kwa mtu yeyote na akaendelea kunifanyia hivyo nikiwa darasa la tano,”amesema
Shahidi wa pili, ambaye ni mama wa mwanafunzi huyo, aliileza Mahakama kuwa aligundua mtoto wake akifanyiwa kitendo hicho baada ya kujikuna makalioni kila akilala ambapo siku moja alimuuliza na kumweleza kuwa huwa anaingiliwa na mwalimu huyo sehemu hiyo ndipo alipokwenda kituo Cha polisi kigongo felly na kupewa fomu namba 3 ya polisi kisha kwenda Hospital ya Wilaya hiyo kwa uchunguzi.
Shahidi wa nne Dk Mussa Mishamo ambaye ni Mganga wa Hospital ya Wilaya ya Misungwi aliileza Mahakama kuwa Novembe 23 mwaka Jana alimfanyia uchunguzi mtoto huyo na kubaini sehemu zake za haja kubwa zimepanuka na kuwa wazi tofauti na kawaida.
Akijitetea kabla ya kusomewa hukumu, mwalimu huyo aliiambia Mahakama yeye kama kama mwalimu asingeweza kumfanyia kitendo hicho mtoto huyo.
Mwendesha mashitaka wa polisi, Ramsoney Salehe aliiomba Mahakama kutoa adhabu kali ili iwe fundisho wa wengine akidai aliyefanya kitendo hicho ameaminiwa na wazazi kwa kulea watoto lakini amefanya vitendo ambayo havikubaliki kwenye Jamii.