Wasanii wanaounda kundi la @Mabantuofficial kupitia akaunti za kurasa zao za mitandao ya kijamii wametangaza kuachia EP yao ifahamikayo kama ‘University EP’ itakayoachiwa siku ya kesho Machi 28.
EP hiyo ina ngoma 8 na Mabantu wamesema itakua na burudani ya kutosha, elimu na vya kujifunza ndio maana wameita University EP.
‘Hii Ni Zawadi Yetu Kwenu #UniversityEp Tunaimani Utakacho Enda kukiskia Kwenye Hii Ep Yetu Ya #UniEp Au #UniversityEp Ni zaidi Ya Burudani Ya Kiwango Cha Juu na yenye Elimu Ndani Yake Ndiomana Kwa Heshima na Taadhima Tuikaipa Hadhi Ya Jina la UniversityEp Coz Tunaimani Yapo Ya kuburudisha, Kuelimisha na Kujifunza kwenye #UniversityEp So Kwa heshima Na Taadhima Tunaomba Utukabidhi Sikio na macho yako Kwenye Hii Ep Yetu Ambayo Rasmi inatoka 28.03.2023 siku Ya Kesho Jumanne Asubuh Asanteh
#UniversityEp #universityEpByMabantu #UniEp #nomabantunovibe #streetking