Homa ya Dengue imesambaa katika Mji Mkuu wa Sudan, Khartoum kwa mara ya kwanza tangu kuingia kwa ugonjwa huo nchini humo.
Tangu Julai mwaka jana homa hiyo ambayo imeenea sehemu mbalimbali nchini humo imekwisha sababisha vifo vya takribani watu 45.
Homa hiyo huenezwa na mbu na dalili zake ni pamoja na homa kali, maumivu ya kichwa na maumivu ya misuli.
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa tahadhari kuwa kile ambacho hospitali za Sudan zinakiona kwa sasa ni kidogo sana sababu wagonjwa wengi huwa hawaendi hospitali wakati dalili zao zikiwa si kali.
#KoncepttvUpdates