Bodi ya Msamaha kwa wafungwa nchini Afrika Kusini itazingatia iwapo nyota wa zamani wa Michezo ya Olimpiki ya Walemavu aliyepatikana na hatia ya mauaji Oscar Pistorius anaweza kuachiliwa kutoka jela.
Hadi sasa ametumikia nusu ya kifungo chake cha miaka 13 kwa kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp mwaka 2013.
Iwapo atapewa msamaha, Pistorius, ambaye sasa ana umri wa miaka 36, anaweza kuachiliwa ndani ya siku chache.
Hata hivyo, mamake Bi Steenkamp, June, anatarajiwa kupinga msamaha wakati wa kusikilizwa kwa kesi Ijumaa.
Mwanariadha huyo wa zamani aliyekatwa mguu kwa sasa yuko katika gereza lenye ulinzi duni katika viwanja vya rolling nje kidogo ya jiji la Pretoria.
Hivi majuzi alikutana na Barry Steenkamp, babake Reeva, kama sehemu ya mchakato wa lazima unaojulikana kama “mazungumzo ya mwathirika na mkosaji”.
Lakini Bi Steenkamp ameweka hadharani kusikitishwa kwake kwamba mshindi huyo wa medali ya dhahabu mara sita kwenye Olimpiki ya Walemavu – huku akionyesha majuto makubwa kwa kumuua mpenzi wake katika Siku ya Wapendanao mwaka 2013 – anaendelea kushikilia kuwa alimpiga risasi kimakosa, akiamini kuwa alikuwa jambazi.o