RAIS wa awamu ya 45th wa Marekani Donald Trump amewashutumu wapinzani wake wa kisiasa kwa kutumia mfumo wa haki wa Marekani kumuondoa “mgombea mkuu wa chama cha Republican” katika uchaguzi ujao, kufuatia uamuzi wa mahakama kuu ya Manhattan kumfungulia mashtaka.
“Watu wa Marekani wanatambua haswa kile ambacho Wanademokrasia wa Kushoto wanafanya hapa,” Trump alisema katika akaunti yake ya Truth Social, Alhamisi.
Aliwasihi wafuasi wake kubaki na umoja ili “kuwafukuza kila mmoja wa Wanademokrasia Wapotovu ofisini.” Baraza kuu la mahakama lilipiga kura Alhamisi kumfungulia mashtaka Trump katika kesi inayohusu malipo ya kimyakimya ya dola 130,000 yaliyotolewa kwa mwigizaji wa picha za wakubwa Stormy Daniels kupitia kwa wakili wake Michael Cohen.
Trump amekuwa akikana jambo hilo na ufahamu wowote wa malipo hayo, na kuonya kuhusu madhara yanayoweza kutokea iwapo atakamatwa.