Kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu hapa nchini, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi mpya na mabadiliko ya vituo vya kazi kwa mabalozi wawili hii leo.
Mabadiliko hayo yamehusisha kubadilihiowa kwa Balozi Humphrey Polepole kutoka kuwa muwakilishi wa nchi huko Malawi na kuiwakilisha Nchi yetu huko nchini Cuba.
Vivo hivyo akimteua Lt. Jenerali Mstaafu Yacoub Mohamed kuiwakilisha Tanzania katika Falme za Kiarabu (UAE) ambaye awali alikuwa akiiwakilisha nchi huko Uturuki.
Akimalizia na uteuzi wa Bw. Iddi Bakari kuwa Balozi na Kumpangia ubalozi wa nchini Uturuki