Mshambuliaji wa klabu ya Kagera Sugar na timu ya taifa ya Tanzania
Anuary Jabir amewasili Nchini Ubelgiji kwa ajili ya majaribio ya wiki mbili katika klabu ya Gent inayoshiriki Ligi Kuu Ubelgiji ambapo wapo nyota wengine wa Tanzania, Mbwana Samatta (Genk), Novatus Dismas (Zulte Waregem) na Kelvin John (Genk)
“Striker him self ANUARI JABIR @anuarjr25 amepata mualiko wa Wiki mbili kutoka Club ya Ligi kuu ya Ubelgiji (Pro League Belgium) #KAAGENT kwa ajili ya majaribio ya kuchezea timu hiyo.
Anuari amewasili leo asubuhi na muda wowote ataanza majaribio.
Club inamtakia kila la kheri na kumuombea mafanikio katika majaribio hayo” Taarifa kutoka Klabu ya Mtibwa Sugar FC