

Mafunzo hayo ya wiki moja yanaendelea katika mikoa ya Mwanza na Arusha yakiendeshwa kupitia Chuo cha Usimamizi wa Bima na Hifadhi ya Jamii Afrika (ACISP).
Wakizungumzia hatua hiyo Mkurugenzi wa Wateja binafsi wa Benki ya NBC, Bw Elibariki Masuke pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Britam Tanzania Bw Raymond Komanga walisema mafunzo hayo yanalenga kupanua wigo wa utoaji wa huduma za bima nchini kutokana na ukubwa wa mtandao wa makala wa benki hiyo kote nchini.
“Kupitia mafunzo haya tunakwenda kuongeza wigo wa watoa huduma za Bima nchini hasa kwa kuzingatia kwamba NBC tayari tuna mtandao wa mawakala 10,000 kote nchini ambao kupitia mafunzo haya watajengewa uwezo na kupatiwa vigezo vitakavyo wawezesha kutoa huduma za Bima pia.’’
“Ni fursa kwa mawakala wetu kuongeza kipato kwa kuwa sasa hawatafanya tu miamala ya kibenki bali pia wataanza kufanya miamala ya kibima na na hivyo kujiongezea kipato kupitia ‘kamisheni’,’’ alisema Bw Masuke.
Hatua hii ni muendelezo wa mkakati wa Benki ya NBC katika kusogeza zaidi huduma zetu karibu na wananchi ikiwa ni muitikio wa wito wa Serikali unaohamasisha taasisi za fedha nchini kusogeza zaidi huduma zetu ili ziweze kuwafikia wananchi wengi zaidi.