Meneja wa Manchester United Erik ten Hag anaona nahodha wa Uingereza Harry Kane kama chaguo lake la kwanza la mshambuliaji msimu huu lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 yuko tayari kusajiliwa katika mkataba mpya Tottenham. (Athletic – subscription required)
Beki wa Uingereza Harry Maguire, 30, atauzwa United msimu huu huku Ten Hag akitoa wito kwa klabu hiyo kuwa na jeuri zaidi katika kukiondoa kikosini. (Manchester Evening News)
Manchester United wamefanya mazungumzo ya kiuchunguzi kuhusu kumsajili beki wa pembeni wa Ufaransa Benjamin Pavard, 27, kutoka Bayern Munich. (Athletic – subscription required)
United wameanza mazungumzo juu ya kumsajili beki wa pembeni wa Bayer Leverkusen na Uholanzi Jeremie Frimpong, 22. (Florian Plettenberg)