Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt. Samia Suluhu amefanya teuzi ya viongozi wafuatao kukaimu nafasi ya wenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi na wenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Taifa.
Amemteua Bw. Adrew Wilson Massawe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Tafiti za Kilimo Tanzania (TARI).. Bw Massawe amekaimu nafasi aliyokuwa Dkt. Tausi Mbaga Kida aliyeteuliwa kuwa Katibu mkuu, Ofisi ya Rais Uwekezaji.
Aidha amemteua Prof. Ulitenga Obadia Lebson Mbamba kuwa mwenywkiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).
Uteuzi huo ulianza rasmi 23 Machi, 2023