Klabu ya Chelsea imefikia makubaliano ya kumteua aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Frank Lampard kuwa kocha wa muda/mpito kwa mkataba mpaka mwisho wa msimu huu na kuchukua mikoba ya Graham Potter aliyefutwa kazi.
Lampard raia wa England aliyewahi kuichezea Chelsea na kuiongoza kushinda ligi ya Mabingwa Ulaya mnamo 2012 kama nahodha amekubali kuchukua nafasi hiyo huku Chelsea wakiendelea na mchakato wa kusaka kocha mkuu mpya wa muda mrefu.