Rubani Rudolph Erasmus wa Afrika Kusini, amepongezwa kwa kufanikiwa kutua kwa dharura baada ya kuona nyoka aina ya fira (Cape cobra) akiwa amejikunja chini ya kiti chake. Erasmus alikuwa akisafirisha abiria 4 kutoka Cape Town kuelekea mji wa kaskazini wa Nelspruit juzi Jumatatu asubuhi.
“Nilipogeuka kushoto kwangu na kutazama chini, niliona nyoka wa aina ya fira (Cape cobra) akirudisha kichwa chake chini ya kiti changu,” alinukuliwa akisema. Rubani huyo aliwaambia abiria wake kwamba “Sikiliza, kuna shida. Nyoka yuko ndani ya ndege. Ninahisi kuwa yuko chini ya kiti changu kwa hiyo itabidi tutue ardhini haraka iwezekanavyo. Hata hivyo wahandisi walioipokea ndege hiyo hawakumpata nyoka huyo” alisema Bw Erasmus​
Credit; BBCÂ