
Ruvu na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira Morogoro (MORUWASA) wamekutana mkoani Morogoro na kukubaliana kuongeza ushirikiano katika kuhakikisha uwepo wa maji safi, salama yenye kutosheleza, kwa matumizi ya nyumbani na usafi wa mazingira.
Pia kuhakikisha jukumu la kulinda rasilimali za maji na utoaji wa elimu ya kutunza vyanzo vya maji linakuwa shirikishi kwa wanufaika wa jumuiya za watumia maji.
Mwenyekiti wa Bodi ya Maji, Bonde la Wami-Ruvu Bi.Hafsa Mtasiwa amesisitiza kuainishwa kwa mipango endelevu ya pamoja kama vile uchimbaji wa mabwawa na upandaji wa miti rafiki kwa maji kwenye vyanzo vya maji kwa ajili ya kurejesha uoto wa asili katika mkoa wa Morogoro.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) Prof. Romanus Ishengoma kuhusu hilo amesema kuwepo na vikao vya mara kwa mara baina ya taasisi ili kuimarisha kufanya kazi pamoja.
Aidha amesisitiza kuwa Bodi yake ipo tayari kulipa kwa haraka tozo za matumizi ya maji kwa kila mwezi ili kuhakisha shughuli za utekelezaji wa usimamizi wa vyanzo unafanyika kwa wakati.
Bodi zote mbili zimekubaliana kuzishirikisha mamlaka za Mkoa na Halmashauri katika maeneo ya vyanzo vya maji yenye changamoto za uvamizi wa shughuli za kibinadamu kama kilimo, mifugo, ukataji wa miti kwa ajili mbao na mkaa vinapatiwa ufumbuzi wa haraka.
