Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Angellah Kairuki, amesema katika mwaka wa fedha wa 2023/24, Ofisi ya Rais -TAMISEMI imetengewa shilingi bilioni 16.58 kwa ajili ya ununuzi wa magari 81 katika ofisi za wakuu wa mikoa.
Kati ya magari hayo, magari matano ni ya wakuu wa mikoa, magari mawili ni ya makatibu tawala wa mikoa na magari 74 ni ya wakuu wa wilaya.