Ikiwa zimesalia siku 2 kuelekea mechi ya watani wa jadi kutokea Kariakoo wakiwa wanaunda KARIAKOO DERBY, klabu ya Simba SC yaonyesha mzuka kwa tambo na mazoezi zaidi kudhihirisha kuwa inaitaka zaidi mechi hio ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara itaowakutanisha wao na wapinzani wake wa karibu yaani klabu ya Yanga (Wanajangwani) kuibuka na Ushindi wa kishindo mnamo tarehe Aprili 16 Mwaka huu.
Derby hio ya Kariakoo imekuwa ikizunguzmziwa zaidi kutokana na wimbi kubwa la mashabiki huwa na hurka ya kushabikia Simba au Yanga tangu miaka mingi hapo nyuma.
Ikichagizwa na namna wasemaji (Maafisa Habari na Mawasiliano) wa klabu husika kupitia misemo yao ya majigambo zaidi huongeza chachu ya kuonyesha nani anaitaka zaidi mechi husika kwa kuibuka na ushindi.
Ukifuatilia kwa ukaribu utagundua Afisa Habari wa Simba Ahmed Ally anaeleza kuwa Inahitajika klabu yake kuikumbusha Yanga SC nafasi yake (Status) katika soka hapa nchini.