
Utamaduni wa namba za magari Dubai kuuzwa kwa bei ya juu sana pengine kuliko hata gharama za magari mengi tu ya kifahari unazidi kushika kasi ambapo kwenye habari za wiki Dubai ime-trend na ‘plate number’ iliyouzwa mnadani kwa kiasi cha dirham milioni 55 ( USD milioni 15) ambayo ni zaidi ya bilioni 35 kwa pesa za Tanzania.
Waandaaji wa Mnada huo “Emirates Auction” wamesema bei ya namba hiyo ambayo ni P7 imevunja rekodi ya awali iliyoshikiliwa na Mfanyabiashara Saeed Abdul Ghaffar Khouri ambaye mwaka 2008 alinunua plate number ya gari kwa USD milioni 14.2 katika mnada ulioandaliwa na kampuni hiyo hiyo.
Mapato yaliyopatikana kwenye mnada huyo yamepelekwa kwenye kampeni ya “One Bilion Meals” kampeni inayoendeshwa na Mtawala wa Dubai Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum na Waziri Mkuu wa UAE ili kusaidia jamii zilizokumbwa na changamoto mbalimbali duniani wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Namba za magari zenye tarakamu chache ikiwemo zenye tarakimu moja Dubai zimekuwa kwenye utamaduni wa kuuzwa kwa bei ghali zaidi na huwa zina ufahari na kuwatambulisha Matajiri kwa njia ya kipekee kwani wenye pesa ndefu tu ndio wenye uwezo wa kuzinunua.
#koncepttvupdates