
Benki ya NMB ikiwa katika muendelezo wake wa kutaka kukamilisha kampeni yake inayofahamika kama MitiMilioni iliyoanzishwa rasmi mwezi Aprili na ambayo ilifunguliwa na Makamu wa Rais wa hapa chini Mh Dkt. Philip Mpango bado ianendelea kujikita katika kupiga hatua ya kukamilisha vyema kampeni hio.
Juhudi za kupambana na athari za mabadiliko ya tabia nchi zinaendelea kupitia kampeni yake ya #MitiMilioni nchi nzima na leo, tumepanda miti zaidi ya 3,000 katika kambi ya Magereza Kazima – Tabora.
Zoezi hili la upandaji miti lilioongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora – Dkt. Rogath Mboya aliyeambatana na viongozi mbalimbali,
Afisa Mkuu wetu wa Rasilimali watu – Emmanuel Akonaay, Kaimu Meneja Kanda ya Magharibi – Ferdinand Mpona pamoja na wenzetu kutoka kanda ya Magharibi.

