Golikipa nambari 3 wa Klabu ya Simba amejivunia akiwa Bado kinda katika Kikosi hicho ameweza tayari kujiwekea rekodi Nzuri ya Kuwa na “Clean Sheets” 2 katika michezo miwili mikubwa lakini hasa Mechi yao dhidi ya Yanga (Kariakoo) iliyochezwa Aprili 16, 2023.
Kinda huyo ametuma Salamu za Shukrani kwa Magolikipa wenzake ambao ni wazoefu katika shughuli hio tangu kitambo yaani Aishi Manula (kipa nambari 1) na Beno Kakolanya (Kipa nambari 2) kwa namna wanavyompa ushauri na kumtia moyo wa uthubutu.
“Kwanza kabisa namshukuru mwenyezi Mungu kwa kunijalia cleansheet pili nawashukuru makipa wenzangu Beno na Aishi kwa kunijenga zaidi na pia nawashukuru bench la ufundi kunipa nafasi mwisho kabisa nawashukuru sana mashabiki wa simba kwa upendo wenu karibuni ukurasa wangu wa twiter”
#koncepttvupdates