Mkuu wa Wilaya mpya wa Kilosa, Hamdu Shaka kwa niaba ya Wanakilosa atoa shukurani za dhati kwa Rais Dkt. Samia Suluhu kwa namna alivyoweza kuithamini wilaya hio kwa kuipatia fedha kuwezesha ujenzi wa Barabara.
“Namshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha nyingi kiasi cha shilingi bilioni 32.9 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Rudewa hadi Kilosa. Ni mradi huu umeandikwa katika ilani ya CCM, hivyo ni utekelezaji wake ni utekelezaji wa ilani” Shaka Hamdu Shaka, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa
“Kukamilika kwa barabara ya Rudewa -Kilosa itakwenda kuimarisha hali ya uchumi wa Kilosa, uchumi wa wananchi na mwananchi mmoja mmoja na Kilosa itakwenda kubadilika kufuatia ujio wa miradi mikubwa kama hii ya ujenzi wa miundombinu ya barabara” Shaka Hamdu Shaka, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa