Kupitia mkutano na Waandishi wa Habari kelekea Michuano ya Hatua ya Robo Fainali Klabu Bingwa Barani Afrika, Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC Afunguka tambo hizi dhidi ya klabu pinzani Wydad Casablanca wanaotarajia kukutana naye siku chache za usoni.
“Wydad tunaenda kumfanyia balaa, hawataamini. Dhamira yetu ni kuvunja mwiko wa kuishia robo fainali, kumtoa Wydad. Tunakiri wametuzidi ubora lakini tunaamini tunakwenda kuwatoa. Safari hii tunaitaka nusu fainali.”- Ahmed Ally.
“Mechi ya Simba na Wydad ndio mechi kubwa barani Afrika wiki hii sababu tunakutana na bingwa mtetezi lakini pia watu wanataka kuona Mnyama akivunja historia ya mwaka 2003 kumtoa bingwa mtetezi.”Ahmed Ally.
“Lazima tukawaadhibu Wydad, lazima tuwaonyeshe yaliyomo yamo. Itakuwa ni siku ya Eid siku hiyo, njoo umeshiba pilau lako, umewaka uje tuhakikishe Wydad wanakaa” Ahmed Ally.