RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt. Samia Suluhu Hassan amempongeza Mwanariadha Gabriel Geay kwa kuiwakilisha nchi vyema katika Mashindano ya Riadha ya Kimataifa ya Boston, kutokana na Mkata upepo huyo mwenye asili ya nchini Tanzania aibuka Nafari ya Pili katika Mashindano hayo.
“Nakupongeza Gabriel Gerald Geay kwa kuwa mshindi wa pili katika Mashindano ya Riadha ya Kimataifa ya Boston yaliyofanyika leo nchini Marekani. Jitihada zako zimeijengea heshima Tanzania. Nakutakia kheri katika kusonga mbele zaidi. Serikali itaendelea kuwaunga mkono wanamichezo”. #Repost @samia_suluhu_hassan
・・