Mkurugenzi wa kampuni ya MyFish Tanzania,iliyopo Kata ya Luchelele wilaya ya Nyamagana mkoa wa Mwanza Mpanju Elpidius inayojihusisha na ufugaji wa samaki ndani ya Ziwa Victoria kwa njia ya vizimba amewataka vijana kufanya ufugaji wa samaki kwa njia hiyo ili wajipatie kipato.
“Aprili mwakani tunatarajia kuwa na watumishi 100,kuwa na vizimba vya kufugia samaki 200 ambavyo vitakuwa vinazalisha samaki tani 200 kwa mwezi,hii ni fursa nzuri kwa Watanzania kutumia nyama nyeupe ambayo ni samaki”
“Tunatarajia kuongeza kiwango cha uzalishaji wa samaki kufikia hadi tani 1200 kwa njia ya vizimba kwa mwaka ambazo zitazalishwa katika shamba hili la Ziwa Victoria”Mpanju Elpidius Mkurugenzi wa kampuni ya MyFish Tanzania