Mfanyabiashara maarufu nchini, Fred Vunjabei Amefunguka kupitia Ayo TV_ baada ya Manispaa ya Mkoa wa Mjini Magharibi kuvunja ngazi ya kupandia dukani kwake kwa kinachodaiwa zimewekwa bila kufuata utaratibu ambapo amesema hakuweza kufanya lolote wakati inavunjwa kwakuwa alikuwa akijianda kutazama Derby ya Simba na Yanga iliyochezwa jijini Dar es Salaam.
Fred amenukuliwa akisema “Tunacholalamika sio kuondolewa ngazi hatuwezi kuzibishia Mamlaka ,tunacholalamika ni namna ngazi ilivyoondelewa kwasababu wangeweza kutupa masaa matatau au sita, wangesema mmekosea hii ngazi imegusa eneo la wapita njia tungeweza kubadilisha”
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mjini Unguja Idrissa Kitwana amesema amesikia kilichotokea na tayari amewataka Manispaa kukaa na Fred na kutazama utaratibu mzuri usioathiri mipango miji.