Kilimo cha Zao la Vanilla nchini Tanzania kimekuwa sio kigeni sana kusikika masikioni mwa watu wengi, hio ni kutokana na usambazwaji wa taarifa nyingi zihisianazo na aina hio ya kilimo hapa nchini.
Zao la Vanilla ni Maarufu sana Duniani kwote kulingana na kuwa na soko na bei nzuri kuhusiswa zaidi katika mauzo yake katika miaka ya hivi karibuni kutokana na uhitaji wake kuongezeka maradufu ya matumizi yake ya hapo awali.
Ukiachana na jitiada zinazofanywa na Wizara ya Kilimo ya nchini Tanzania katika kuhamasisha kilimo hicho cha Zao la Vanilla kulikuwa bado na mwamko mdogo sana wa watu kuamini na kuwekeza zaidi katiaka aina hio ya kilimo kwani hakikuonesha tija ya moja kwa moja kwa kudhihirisha soko lake na mapato, hivyo Kampuni ifahamikayo kwa jina la VANILLA INTERNATIONAL LTD iliyoanzishwa chini ya Mkurugenzi Mtendaji Simon Mnkondya Ilichukua nafasi zaidi ya kukuza uelewa na kujikita katika uwekezaji juu ya Zao hilo.
Vanilla Village Mkoani njombe ndio mradi ulilowahi shika hatamu kwa namna ya kuchagiza uwerkezaji wa Zao hilo lililoaminishwa ni Zao la gharama sana Duniani kwa linalipa haswaa pale pindi ukiwekeza. Mwitikio wa uwekezaji ndani ya mkoa wa Njombe kwa kipindi fulani.
Baada ya muda kupita habari kuhusiana na Vanilla Village Mkoani humo zilikata ghafla na hio ilizua maswali mengi kuhusiana na nini hatima ya mradi huo pasipo kupata majibu.
Wadau wengi wakajawa na wasiwasi na kuanza ona aina ya mradi wa kilimo hicho kuanza kuwa na utata.
Mara umma ukaanza fahamishwa kuwa mradi huo umehamishiwa Visiwani Zanzibar na baada ya Muda ukafunguliwa pia katika Jiji la Arusha, hapo uakazuka utata kutaka fahamu je wale waliowekeza Njombe Village walishia wapi juu ya uwekezaji katika kilimo hicho.
Mahojiano yalifanyika jijini Arusha kuptia U TV iliyochini ya Azam Media, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya VANILLA INTERNATIONAL LTD Simon Mnkondya ameweka bayana kuhusu sababu kubwa iliyochangia mradi huo kuhamishiwa Zanzibar na pia Arusha
Ameeleza kuwa Mradi wa Vanilla mkoani Njombe ulienda vizuri, zao la vanilla lilistawi vizuri sana ila iliposhuka Barafu katika sehemu ya Majira ya Mwaka yaani mwezi wa 7 ndipo imepelekea kufanya maamuzi ya Kufanya utaratibu wa Kuhamisha kituo cha Uwekezaji na Kuelekea Zanzibar.
Aidha ameongeza kuwa kampuni hio ina Bima ambayo imesaidia kuwalipa Wadau waliowekeza katika mradi wa Vanilla mkoani Njombe kwa zaidi ya Asilimia 99. Kwasasa Mradi huo umewekezwa zaidi Visiwani Zanzibar na Arusha, Wadau wengine wamepewa maeneo mapya