Klabu ya Yanga inatarajia kuanza Safari yake hapo kesho Alhamisi ya Aprili 20 kuelekea nchini Nigeria kwa lengo la kukichapa vikali dhidi ya Rivers United katika hatua ya Robo Fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
“Kikosi kitaondoka Dar es Salaam kesho alfajiri na shirika la ndege la Ethiopia kuelekea Nigeria kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali #cafconfederationcup dhidi ya Rivers United utakaochezwa kwenye Jimbo la Akwa Ibom Kusini mwa Nigeria” Ally Kamwe