
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Geita ACP Safia Jongo amesema mpaka sasa wanaendelea kumsaka mtu huyo huku chanzo cha tukio hilo ni tamaa za mali ambazo zilikuwa zikimilikiwa na Mama huyo .
“Kiini cha tukio hili ni tamaa ya Mali na nichukue nafasi hii kutoa wito kwa jamii tutafute kwa jasho letu kila siku naendelea kusema kwamba matukio kama haya ni matukio ya kutokuwa na hofu ya Mungu, ” -ACP Jongo.
ACP Jongo amesema Baba huyo amekuwa akiishi Nyumbani kwa Mama huyo ambaye kwa sasa ni Marehemu pamoja na watoto ambao sio wa kwake na huyo mama alikuwa ni mtafutaji ambaye alikuwa akimzidi Baba huyo kipato.