
Agizo hilo limetolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe, Theopista Mallya wakati akiongelea kuhusu ukaguzi wa magari ya kubebea Wanafunzi katika Mkoa huo ambao amesema agizo hilo linatokana na baadhi ya Madereva kuwafanyia Watoto vitendo vya ukatili ikiwemo kuwabaka ambapo gari likiwa na tinted inakuwa vigumu kuwagundua Madereva hao.
Kamanda Theopista amesema magari yote ya Shule katika Mkoa huo lazima yawe na vioo vinavyoonesha ili iwe rahisi kubaini makosa ya Madereva ikiwamo wanaowapakata Watoto na kuzidisha idadi ya Wanafunzi.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani Mkoa wa Songwe (RTO), Charles Bukombe amesema wametoa siku moja kwa Wamilmi wa magari hayo yenye vioo vyeusi kuviondoa ambao baada ya hapo magari ya kubeba Wanafunzi ambayo yatakuwa bado na vioo vyeusi yatakamatwa.