Rapa kutokea nchini Tanzania ambaye kwa sasa yupo nchini Marekani @Roma_Mkatoliki ameachia wimbo mpya unaoenda kwa jina la “Nipeni Maua Yangu” ambao hakika umekuwa gumzo mtandaoni kupitia aina ya mashairi aliyoweka katika wimbo huo.
Baada ya wimbo huo ku-trend sana na kuwafikia wengi, watu wamekuwa na maoni na mitazamo tofauti ya kusema kuhusiana na mashairi ya wimbo huo.
Baadhi ya Viongozi wa Kisiasa wamemshauri Msanii huyo aweze kurejea nchini kwake kwa kumtoa hofu kuwa hali ni nzuri chini ya Uongozi wa awamu ya 6 nchini Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan
Hizi ni niongoni mwa tungo za mashairi yanayopatikana katika wimbo wake mpya #NipeniMauaYangu
“Tatizo mkishaapishwa tuu mnawaza uchaguzi ujao,hamuwazi njia mbadala ya kumlinda mkulima na mazao sasa Iringa si kuna msitu halafu Toothpick tunaagiza China make kwanza hapo nicheke” @Roma_Mkatoliki
“Mimi sio CCM wala CHADEMA, simwamini mtawala na mpinzani simsadiki, maana wanaendelea kukatika huku DJ kauzima mziki” @Roma_Mkatoliki #NipeniMauaYangu