Shirikisho la soka barani Africa (CAF) limemteua Msenegali Issa Sy kuwa mwamuzi wa mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Africa kati ya Simba SC na Wydad AC ya Morocco.
Sy anasifika kwa umahiri wa kumwaga kadi kwa wachezaji uwanjani. Takwimu zinaonyesha katika michezo 15 iliyopita aliyochezesha kwenye michuano ya vilabu barani Afrika, ametoa kadi 70. Kati ya hizo 67 zikiwa za njano na 3 nyekundu.