Takriban watu 78 wamefariki katika makabiliano yaliyotokea katika shule moja katika mji mkuu wa Yemen Sanaa wakati wa ugawaji wa chakula cha msaada kwa ajili ya Ramadhan, wamesema maafisa.
Picha za televisheni zilionyesha umati wa watu wakishindwa kusoing na wengi katika hali mbaya katika eneo la mji wawa Sanaa la Bab al-Yemen.
Mamia ya watu waliripoti kuhusu umati wa watu kuingia ndani ya shule ya Maeen School Jumatano jioni kupokea msaada wa wenye thamani ya hadi $9 (£7; €8) kwa kila mtu.
Vuguvugu la waasi wa Houthi linaudhibiti mji wa Sanaa tangu mwaka 2015.
Video zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha watu wakipiga mayowe huku makumi ya miili ilionekana chini, baadhi yao wakiwa hawatikisiki. Watu wengine wanaonekana wakijaribu kusaidia.
Wafanyabiashara mjini huo ambao walipanga tukio hilo la utoaji wa misaada wamekamatwa na uchunguzi unaendelea kuhusu tukio hilo, imesema wizara ya mambo ya ndani.