Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Jenista Mhagama amewataka wataalam kushirikiana na wakandarasi kuhakikisha ujenzi wa Mnara wa Mashujaa unakamilika katika ubora, ambapo shilingi Bilioni moja itatumika kwa awamu ya kwanza ya ujenzi huo.
Jitihada hizo zinafanywa na Serikali ikiwa ni sehemu ya kuenzi na kutunza kumbukumbu inayotambua mchango wa Mashujaa hao waliokuwa wazalendo ksaatika kulipiagania taifa hili na kupelekea nchi kuanza piga hatua ya maendeleo.