Kocha Mkuu wa Wydad Casablanca, Juan Carlos Garrido akizungumzia mchezo wao wa Utakaochezwa hii leo dhidi ya Simba kwenye Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, amekiri ugumu wa mchezo huo licha ya malengo yao kuwa ushindi.
Licha ya timu hio kusalia kuwa ndio Bingwa mtetezi wa Kombe la Klabu Bingwa Afrika bado wanatambua uwezo alionao mpinzani (Simba SC) huyo anayekutana nae katika Mchuano mkali hatua ya Robo Fainali (Quarter Final).
#KoncepttvUpdates