Simba SC yaibuka na ushindi wa Goli 1-0 dhidi ya Bingwa Mtetezi wa Kombe hilo la Klabu Bingwa Barani Afrika Wydad Casablanca AC.
Jean Baleke ameifungia klabu hio Bao la Kipekee ambalo lilisalia hadi dakika 90 kukamilika na kuwafanya wabakie washindi katika mchezo huo wa mkondo wa kwanza wa Hatua ya Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika uliochezwa Aprili 22, 2023 katika Dimba la Benjamin Mkapa uliopo jijini Dar es Salaam