Mkuu wa wilaya ya Musoma Dkt. Khalfany Haule amesema uchunguzi wa madai ya maiti ya mtoto kugeuka jiwe umebaini kuwa mwanamke Amina Abdallah aliyesingizia kuwa mtoto wake amefariki na kugeuka jiwe ni uongo
Amesema mwanamke huyo alifanya hivyo kwa lengo la kumridhisha Mmmewe Hamis Juma kwa kuwa mwanaume huyo alihitaji mtoto wa kiume na yeye alizaa mtoto wa kike
Imeelezwa kuwa Amina alikuwa na makubaliano na Hamisi ya kumzalia Mtoto wa kiume tangu mwanzo wa mahusiano yao hivyo Hamisi akaendelea kulea mimba akitarajia Mtoto wa kiume, baada ya kujifungua Mtoto wa kike, Amina aliendelea kumwaminisha Hamisi kuwa amejifungua pacha wa kike na kiume
Amina Abdallah aliamua kuokota jiwe na kulipeleka kwa Wakwe na kuzusha alizaa Mapacha lakini Mtoto wa kiume amegeuka jiwe huku akitaka lizikwe haraka kuondoa mikosi.