Paris St-Germain wanafikiria kumuuza Neymar msimu huu wa joto – huku Chelsea na angalau klabu nyingine moja ya Premier League ikitafakari kumnunua mshambuliaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 31 (Mirror)
Mshambulizi wa PSG Lionel Messi anataka kurejea Barcelona lakini klabu hiyo ya Uhispania inahitaji kuongeza pauni milioni 88 kupitia mauzo ya wachezaji na kuamsha ‘kichocheo kingine cha kiuchumi’ ili kumsajili tena nahodha huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 35 (Mail)