Mkuu wa mkoa wa Mara Meja jenerali Suleiman Mzee ametoa siku 3 kwa mkurugenzi wa Manispaa ya Musoma Kukarabati miundombinu ya stendi ya Musoma katika eneo la Bweri endapo watashindwa ukaratabati huo atazuia wafanya biashara wanaotumia stendi hiyo kulipa ushuru.
“Nimesikitishwa na ubovu wa standi hii ya Bweri kwanza Kuna chafu katika eneo hili hata Usimamizi tu hauridhishi kabisa Kama mtashindwa kuanza kwa wakati nakumaliza nitazuia watu wasilipe ushuru wa hapa haiwezekani hatutavumiliana kwa mambo kama haya”Meja jenerali Suleiman Mzee Rc Mara