
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ameyasema hayo alipojumuika kwa chakula cha Eid El Fitri na watoto 628 wanaolelewa katika vituo 7 kutoka mkoani Dar esalaam na kimoja Wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani Aprili 23, 2023.
“Nafahamu, vituo hivi pamoja na mafanikio, vinapitia changamoto mbalimbali ikiwemo; upungufu wa vyakula na vifaa vya shule kwa wanafunzi; kukosa mahitaji muhimu kwa wakati; malazi na mavazi. Hivyo, Serikali tutakua sehemu ya kuwapatia ushauri pale inapohitajika kwa kuungana na wadau mbalimbali wa maendeleo, tutashirikiana kutatua baadhi ya changamoto hizi ili tuweze kufikia malengo”. Amesema Waziri Dkt. Gwajima.
Amewapongeza Wadau wote nchini wanaogusa watoto wa kundi hilo na kuwaomba wananchi kuendelea kujitokeza kuwafikia watoto wenye uhitaji popote walipo.
“Kazi yenu inahusu kusimika maadili na tabia njema za watoto hawa zitakazowaandaa kuwa viongozi wa kesho na vijana wenye manufaa kwa taifa. Natambua, malezi kwenye zama za sasa za utandawazi zinahitaji ubunifu mkubwa ili kuvutia akili na fahamu za watoto kupokea na kujiamini kwenye kuyaishi malezi hayo hivyo, ahsanteni sana kwa utayari” ameongeza Mhe. Dkt. Gwajima.
Waziri Dkt. Gwajima amewaasa pia watoto hao kuzingatia malezi na elimu kwani kwa ajili ya maisha Yao ya baadaye huku na kujisimamia kwa kuepuka kuingia kwenye makundi rika yasiyo na maadili ikiwa ni pamoja na kujiimarisha kiimani.
Halfla hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya “Chocolate Princess” chini ya “The Mboni Show” imejumuisha vituo vya MAUNGA CENTER, AL-MADINA ORPHANS CENTER, FADHILAH ORPHANAGE CENTER, NEW LIFE ORPHANS HOME, YATIMA GROUP TRUST FUND, HIYARI ORPHANAGE CENTER na MWANDALIWA ORPHANAGE CENTER,

