Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS, Mhandisi Rogatus Mativila amesema, ujenzi wa daraja la Kigongo-Busisi unaendelea vizuri na kwa sasa umefikia asilimia 72 huku ukitarajiwa kukamilika tarehe 25 Februari, 2024. Daraja hilo litakapokamilika wasafiri watakuwa wakitumia dakika 4 badala ya masaa mawili hadi manne wanayotumia hivi sasa kuvuka.
“Daraja la Kigongo-Busisi linafupisha safari kwa kiasi kikubwa sana, ukitoka Mwanza-Geita-Sengerema ni karibu kilometa 210 lakini ukitoka Mwanza na kupitia daraja la Kigongo-Busisi kwenda Sengerema ni karibu kilomita 90” Mhandisi Rogatus Mativila, Mtendaji Mkuu wa TANROADS
Mwonekano wa ujenzi wa daraja la Kigongo-Busisi mkoani Mwanza, ambalo ujenzi wake unaendelea. Kwa sasa ujenzi umefikia 72% na unatarajiwa kukamilika Februari 25, 2024. Baada ya kukamilika, wasafiri watatumia dakika 4 kuvuka tofauti na sasa ambapo wanatumia masaa mawili hadi manne.