Golikipa namabari 3 wa Simba SC Ally Salim amejiwekea Rekodi nzuri katika Michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika baada ya kushiriki michuano hio akiwa bado kinda na umri wa miaka 22.
Anashika nafasi ya Pili Msimu huu katika Ukanda wa Bara la Afrika kuaminika katika kikosi cha timu yake hio ni baada ya kupewa nafasi ya Kulinda Lango katika mechi ya Mkondo wa kwanza hatua ya Robo Fainali dhidi ya Wydad Casablanca kutokea Morocco iliyochezwa nchini Tanzania Aprili 22, 2023.
“Ally Salim ndie mlinda mlango wa pili mdogo zaidi aliyedaka kwenye Robo ya ligi mabingwa Afrika msimu huu akiwa na miaka 22 tuu Mlinda mlango mdogo zaidi ni Mohammed Hadid wa Js Kabylie mwenye miaka 21”- Ahmed Ally
Nafasi ya Kwanza inashiliwa na Golikipa wa Js Kabylie, Mohammed Hadid ambaye ana umri wa miaka 21 tu.