Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Bethaneema Mlay amethibitisha tukio hilo na kusema chanzo cha mauaji hayo bado hakijajulikana na kusema Watu wanne wanashikiliwa kwa ajili ya uchunguzi.
“Tulipata taarifa kwamba huko Mtaa wa Mwatulole Kata ya Buhalahala Tarafa na Wilaya ya Geita Mwanamke mmoja ameuawa na Watu wasiojulikana na Timu yetu ya Makachero walifika eneo lile na na kubaini mwili wake umekatwa maeneo mbalimbali na amepoteza maisha”
Mlay amesema watakapo kamilisha uchunguzi wa kifo hicho watatoa taarifa juu ya waliohusika na mauaji hayo huku akisema kwa mujibu wa waliofika eneo la tukio wanasema alikuwa amekatwa kichwani usoni na mikono yote miwili ambapo mkono wa kulia umeondolewa kiganja”