Mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere umeanza kuonyesha faida baada ya kuzuia mafuriko katika baadhi ya mikoa ya Pwani na Morogoro. Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba akiwa katika ziara ya kujionea ujazaji katika bwawa Aprili 25, 2023 amewaambia waandishi wa habari kuwa zoezi la ujazaji maji kwa kiasi kikubwa imezuia mafuriko yaliyokuwa yakiathiri wananchi.
“Tunafurahi kwamba tayari tumefikia mojawapo ya malengo makubwa ya kuanzishwa kwa mradi huu (kufua umeme wa Julius Nyerere) ambayo ilikuwa ni kuwakinga wananchi dhidi ya madhara yatokanayo na mafuriko”@JMakamba, Waziri wa Nishati
“Kwa mujibu wa takwimu, kiwango cha maji yaliongia wiki mbili zilizopita, ni mengi kuliko maji yaliyoleta mafuriko 2019/2020. Hii maana yake kwa neema ya mvua iliyopo kwa sasa, zile athari za mafuriko zilizokuwepo siku za nyuma hazipo tena. Bwawa hili limeanza kuzaa matunda tuliyotarajia ikiwemo kudhibiti mafuriko” @JMakamba, Waziri wa Nishati
“Kwa sasa ujenzi wa bwawa la Julius Nyerere kwa ujumla uko asimilia 86. Wakati Mhe. Rais @SuluhuSamia anachukua madaraka ya nchi mradi huu ulikua ni asilimia 37″ @JMakamba, Waziri wa Nishati