Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Geita ACP Berthaneema Mlaya amesema kuna tukio lilitokea la Mwanamke mmoja (80) mkazi wa kijiji cha Mwenyegeza Kata ya Nyakagomba Wilaya ya Geita amefariki Dunia kwa kukatwa na kitu Chenye ncha kali kichwani na watu wasiojulikana tukio ambalo limesadikika kuwa na imani za kishirikina.
“Tar 23,April 2023 saa 12 asubuhi kitongoji cha Bugunga kata ya Kakola Wilaya ya Nyang’hwale Mwanaume ajulikanaye kwa jina la Juma Masanja (40) alichomewa nyumba zake mbili na kiini cha tukio hilo alikuwa anatuhumiwa ni mwizi sugu tayari watu watano wanashikiliwa kwa tuhuma za kujichukulia sheria mkononi’Berthaneema Mlaya Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita.
“Tukio Jingine ni kwenye Kijiji cha Tinachi Kata ya Nyawilimilwa kundi la vijana nane walivamia na kuvunja maduka nane ya huduma za kifedha na kuiba jumla ya fedha kiasi cha sh,Milion 31.2 Mali ya watu mbali mbali kabla ya kuvunja maduka hayo waliwashambulia walinzi kwa siraha za jadi na kuwaumiza sehemu mbali mbali tunawataka wananchi kuanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi kukabiliana na tatizo la wizi”Berthaneema Mlaya Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita.
“Tukio jingine ni la mtu mmoja mwanamke ambaye jina alijajulikana alikutwa amefariki Dunia pembezoni mwa Barabara kwenye mtaa wa Mwembeni Kata ya Nyankumbu na tukio hilo hadi sasa alijajulikana chanzo chake tunaendelea kufanya uchunguzi wa kubaini kiini cha tukio”Berthaneema Mlay Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita.