Msafara wa viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) uliokuwa ukielekea Kigoma kwa ajili ya maandalizi ya uzinduzi wa Oparesheni mpya ya chama hicho umepata ajali majira ya saa 8 usiku wa kuamkia leo Aprili 27, 2023 katika kata ya Kigwa Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora.
Waliopata ajali ni Yohana Kaunya, Kaimu Katibu Mkuu Bavicha, Nuru Ndosi, Naibu Katibu Mkuu Bawacha – Bara, David Chiduo, Josephat magambo na Daniel Marwa – Dereva.
Hakuna aliyefariki, wote wanapatiwa matibabu katika Zahanati ya Kigwa B, Wilaya ya uyui.
#KoncepttvUpdates