
Mkataba huo ulioshuhudiwa Katibu wa Wizara hiyo Dk. Natu El-Maamry Mwamba na Balozi wa Japani nchini Tanzania Bw. utasaidia kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) ikiwa ni mkakati wa kununua meli ya kisasa ya uvuvi na miundombinu ya kuhifadhi samaki.
Fedha nyingine katika mkopo huo zitatumika kununua pembejeo za kilimo kama vile mbolea kwa ajili ya wakulima wadogo, utoaji wa mbegu bora na kuongeza uzalishaji wa mazao ya mpunga, ngano na alizeti.
“Tanzania na Japan kupitia Shirika lake la Ushirikiano wa Kimataifa (JICA ), zimetiliana saini mikataba mitatu ya mkopo nafuu na msaada wenye jumla ya Yen bilioni 10.15 sawa na shilingi za Tanzania bilioni 174.8, kwa ajili ya kuendeleza kilimo na uvuvi, ambapo katika sekta ya kilimo, mkopo huo utatumika kununua pembejeo za kilimo ikiwemo mbolea, utoaji wa mbegu bora na kuongeza uzalishaji wa mazao ya mpunga, ngano na alizeti, huku sekta ya uvuvi itanufaika na msaada utakaotumika kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (Taficotz), kwa kununua meli ya kisasa ya uvuvi na miundombinu ya kuhifadhi samaki”, Wizara ya Fedha na Mipango yaeleza

