Waziri wa @MadiniTanzania Mhe. Dkt. Doto Biteko (Mb), amewasilisha Bungeni bajeti ya makadirio ya shilingi 89,357,491,000.00 kwa ajili ya matumizi ya Wizara na Taasisi zake kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 kwa mchanganuo ufuatao;
(i) Sh. 23,172,550,000.00 ikiwa ni fedha za maendeleo.
(ii) Sh. 66,184,941,000.00 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida, kati ya fedha hizo, shilingi 20,307,498,000.00 ni kwa ajili ya Mishahara na sh. 45,877,443,000.00 ni Matumizi Mengineyo