Watu wengi huoa kwa sababu wanahisi ni wakati wa kuoa kwa sababu ya umri. Lakini umri sio hitaji la lazima kwa ndoa; kwa kweli, ndilo hitaji la chini kabisa la kuoa. Kuna mambo muhimu zaidi.
Haya ni baadhi ya mambo ambayo mwanaume anapaswa kuwa nayo kabla ya kuoa:
1. KAZI/BIASHARA
Mwanamume anayetafuta kuoa anapaswa kuwa na kitu cha kufanya; kuanzisha familia kunahitaji bili nyingi, na mwanamume ni ‘mwanaume’ zaidi anapoweza kuweka chakula mezani na mahitaji mengine ya msingi ikiwemo maladhi na mavazi. Ikiwa mwanamume hawezi kukidhi wajibu huu, basi familia itaishi katika machafuko – amani itakuwa lugha ya kigeni katika nyumba hiyo.
2. WAZO LA NANI UNAYEMTAKA
Kabla ya mtu kuoa, anapaswa kuwa na wazo la nani anayemtaka; huwezi tu kuchagua mwanamke yeyote na kumuoa, unapaswa kujua ni nani/nini unachokitaka kwa mwanamke.
3. UFAHAMU WA UNACHOTAKA
Jambo lingine muhimu ambalo mwanaume anapaswa kuwa nalo/kujua kabla ya kuoa ni kuelewa unachotaka ndani ya nyumba. Unataka nyumba yako iweje? Unataka ndoa yako iweje? Unapaswa kuwa na wazo la kile unachotaka katika kuanzisha familia kabla ya kuanza. Kwa kweli, haujengi tu nyumba bila kuelewa unachotaka katika nyumba hiyo. Kwanza kuna dhana ya nyumba, kabla ya mbunifu kuchora mpango. Hali hiyohiyo inapaswa kutumika katika ndoa yako.
4. UKOMAVU
Ndoa ni kwa ajili ya akili zilizokomaa na ikiwa haujafikia hatua hii ya kushughulikia hali kwa ukomavu, basi ndoa sio kwako; haihusu umri, lakini jinsi unavyoweza kujidhibiti na kufanya maamuzi ya busara katika joto la sasa. Nakuwekea kwamba kila anayempiga mke hajakomaa kwenye ndoa.
5. MAONO
Maono ni jambo lingine muhimu ambalo mwanaume anapaswa kuwa nalo kabla ya ndoa; unapaswa kuwa na maono yako mwenyewe na pia maono ya ndoa. Hiyo ndoa inaelekea wapi? Unaelekea wapi? Unahitaji kuwa na maono haya kama mwanaume, kwa sababu mtu asiye na maono haendi popote.
6. UJUZI WA MWANAMKE NA JINSI YA KUISHI NAE
Hiki ni kidokezo kingine muhimu ambacho kila mwanaume anapaswa kuwa nacho kabla ya kuoa. Ikiwa hujui jinsi ya kumtendea mwanamke, basi angalau ujue/ ujifunze jinsi ya kumtendea mwanamke wako, na ikiwa hujui jinsi ya kumtendea mwanamke huyo, basi unahitaji kujifunza kabla ya kumwomba kukuoa.
7. NIA YA KUJITUMA
Ikiwa unajua kuwa hauko tayari kutoa 100% yako ili kuifanya ndoa yako ifanye kazi na hautajitolea kikamilifu, basi ndoa sio yako bado. Lazima uwe na bidii ya kujitolea kabla ya kuingia kwenye ndoa.
Mwanaume hatakiwi kukurupuka tu kwenye ndoa kwa ajili yake, haya ni mambo muhimu anayopaswa kuwa nayo kabla ya kuoa.
CC; mteweledigital.documentaries/swahili