Biriani ya kuku, ni chakula kitamu ambacho hupikwa kwa kutumia mchele, nyama ya kuku, mtindi, vitunguu maji, nyanya, zafarani, pamoja na viungo vingine vingi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika biriani hii ya kuku
Ingredients (Mahitaji)
Maelekezo
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, vitunguu swaumu pamoja na tangawizi, kisha visage hadi utakapo ona vimesagika vizuri. Weka nyanya, majani ya giligiliani, pamoja na limao iliyo kamuliwa, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo wote umesagika vizuri hadi kuwa laini.
Ondoa mchanganyiko huo kutoka kwenye mashine ya kusaga na uweke kwenye kontena kubwa, halafu weka mtindi, garam masala, pamoja na chumvi, kisha koroga vizuri.
Weka vipande vya nyama ya kuku ndani ya hilo kontena na uchanganye vizuri, kisha funika kontena na uweke mchanganyiko huo wa nyama ya kuku kwenye friji kwa muda wa kati ya saa 8 na saa 24.
Chukua zafarani na uziroweke ndani ya kikombe chenye maziwa kwa muda wa dakika 30.
Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka maji kwenye hilo kontena, kisha roweka mchele ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa dakika 30.
Chukua sufuria kubwa. Weka ndani ya hilo sufuria, mchele pamoja na maji uliyotumia kurowekea mchele, kisha weka sufuria hilo kwenye jiko lenye moto mkubwa halafu acha ichemke.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, halafu acha iendelee kuchemka taratibu kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona maji kwenye sufuria yamekaribia kukauka na wali bado haujaiva vizuri. Epua wali, kisha mwaga maji yote yaliyobaki kwenye sufuria na kubakiwa na wali peke yake.
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka ndani ya hilo sufuria, iliki, mdalasini, majani ya mbei, pamoja na binzari nyembamba, kisha kaanga vizuri. Weka vipande vya nyama ya kuku ulivyo viweka kwenye friji pamoja na mchanganyiko wake wote wa viungo uliomo ndani ya kontena, halafu koroga vizuri, kisha zima jiko.
Weka vitunguu maji vilivyokaangwa juu ya nyama ya kuku na usambaze vizuri, kisha weka juu ya hivyo vitunguu maji, majani ya giligilani pamoja na majani ya minti, halafu sambaza vizuri.
Weka wali juu ya majani giligilani na majani ya minti, halafu sambaza vizuri, kisha mimina maziwa yenye zafarani juu ya huo wali.
Funika sufuria vizuri kwa kutumia aluminium foil, kisha weka mfuniko juu ya aluminium foil.
Washa jiko na upike biriani hiyo kwenye moto wa wastani kwa mda wa dakika 25, kisha punguza moto na uendelee kupika biriani hiyo kwenye moto mdogo kwa muda wa saa 1, au hadi utakapo ona biriani imeiva vizuri.
Epua biriani na uweke pembeni. Ondoa aluminium foil pamoja na mfuniko halafu changanya vizuri biriani hiyo, tayari kwa kula.
Baada ya hatua hiyo chakula kinatakiwa kuandaliwa kwa kuwekwa kwenye makasha au hotpots za kuhfazia chakula kisha kupelekwa mahala pa kulia au kusamabaza kwa wateja kama ni sehemu ya biashara.