Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amelitaka Jeshi la Zimamoto kufika kwenye matukio ya uokoaji kwa wakati ili kupunguza athari zinazotokana na majanga mbalimbali. Dk Mpango ametoa agizo hilo wakati akifungua jengo la kituo kikuu cha zimamoto Dar es Salam na kusisitiza kuwa jeshi hilo linadhamana kubwa ya usalama wa watu na mali zao na kupunguza athari zinazotokana majanga ya moto.
Ameaninisha malalamiko ya wateja kwa jeshi hilo ikiwa ni pamoja na kuchelewa kufika katika matukio kwa wakati na magari yao kutokuwa na maji. “Tunapoadhimisha miaka 59 ya muungano hamna budi kujitafakari nilazima kuhakikisha mfumo wenu wa kiutendaji na haswa kutokana na ongezeko la watu na ukuaji wa miji ni lazima kuhakikisha jeshi letu linakuwa imara “ Dk Mpango amelitaka jeshi hilo kujiimarisha zaidi ili kuweza kukabiliana na majanga yakiwemo matetemeko ya ardhi,vimbunga na ajali za barabarani, angani na majini.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto nchini, John Masunga