Jana benki ya Stanbic ilipata fursa ya kudhamini na kushiriki katika kongamano la wadau wa wafanyabiashara wachanga, wadogo na wakati lililoandaliwa na kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, ambapo Mkuu wa Kitengo cha Biashara, wa benki wa benki ya Stanbic Bw.Frederick Max, alieleza huduma maalum zinazotolewa na benki hiyo mahususi kwa ajili ya kutimiza mahitaji na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara nchini.
Huduma hizi zikiwemo:
1.Akaunti ya Mpambanaji – yenye masharti rafiki kwa wafanyabiashara,
2.Biashara Exchange – huduma inayo unganisha wafanyabiashara Tanzania na wasambazaji kutoka China
3.Program ya Stanbic Biashara Incubator inayolenga kutoa elimu na ujuzi wa kuendesha biashara.
4.Stanbic wakala inayorahisisha upatikanaji wa hudumu zetu za kibenki ukiwa popote.
5.Usaidizi wa ufanyaji wa biashara kupitia huduma za kibenki bila mipaka (boardless banking), kununua na kubadili fedha za kigeni (FX), nk.
Pia alielezea kuwa benki ya stanbic imejikita katika kuwezesha wafanyabiashara wadogo kukua, kuingia kwenye masoko shindani na kushiriki katika kujenga uchumi wa Tanzania.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara, wa benki wa benki ya Stanbic Bw.Frederick Max (Wapili Kushoto), akiwa mwanajopo katika mdhahalo na wadau wengine kujadili namna ya kuwezesha biashara changa, za chini, ndogo na za kati kukua haraka.