Klabu ya Soka Azam FC leo hii imemtangaza rasmi Youssouph Dabo kuwa Kocha wao mkuu baada ya kukaa bila Kocha mkuu kwa kipindi cha muda mrefu.
Azam ambayo kwa sasa inashikilia nafasi ya Tatu katika Msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara imemtangaza Kocha huyo ikiwa ni siku chache mbeleni wanaenda kuchuana vikali na Simba SC kwenye mchezo wa Nusu Fainali ya Kuwania kutwaa Ubingwa Kombe la Shirikisho la AZAM SPORTS.